Main Article Content

Mdhihiriko wa nyuso za mwanamke katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (2010) ya said Ahmed Mohammed


Stella Faustine

Abstract

Said Ahmed Mohammed ni miongoni mwa waandishi nguli katika fasihi ya Kiswahili. Katika kazi zake, anazungumzia masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Kwa upande wa utamaduni, anajichomoza kama mtetezi wa wanawake kwa kuonesha madhila mbalimbali anayokumbana nayo katika jamii. Katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke, anatumia dhana ya nyuso kama kibainishi cha namna mwanamke anavyoonekana katika jamii. Aidha, shabaha ya makala hii ni kudhihirisha namna mbalimbali za mwonekano wa mwanamke kama inavyojitokeza ndani ya riwaya hiyo. Uchunguzi na mjadala uliongozwa na Nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika. Data zilipatikana maktabani kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi matini; kisha zilichambuliwa na kuwasilishwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwapo kwa nyuso mbalimbali za mwanamke ambazo zinajitokeza ndani ya riwaya ya Nyuso za Mwanamke kama kibainishi cha namna mwanamke anavyoonekana katika jamii. Nazo ni uwezo katika kufanya uamuzi sahihi, uwezo wa kuongoza, pamoja na uwezo wa kiuchumi.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789
 
empty cookie