Main Article Content

Nafasi ya hadithi katika ukuzaji wa stadi za kusikiliza na kuzungumza: mfano wa shule teule za sekondari wilayani Nyagatare nchini Rwanda


Emilien Bisamaza

Abstract

Makala hii inabainisha nafasi ya hadithi katika kufundishia na kujifunzia stadi za kusikiliza na kuzungumza. Aidha, makala inalenga kuunda mwongozo wa kutumia hadithi kufundishia na kujifunzia stadi hizo. Ukusanyaji wa data ulifanywa kupitia ushuhudiaji, mahojiano na uchanganuzi wa matini. Walengwa wa utafiti walikuwa wanafunzi na walimu wa Kiswahili kutoka shule teule za sekondari katika wilaya ya Nyagatare. Data zilizokusanywa, zilichambuliwa kwa njia ya maelezo. Nadharia ya Utambuzi ndiyo iliyoongoza makala hii. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa hadithi ina nafasi muhimu katika ufundishaji na ujifunzaji wa stadi za kusikiliza na kuzungumza. Hadithi huwavutia wanafunzi, wakawa na motisha ya kujifunza bila uchovu. Kutokana na changamoto zilizoshuhudiwa kuhusu utumiaji wa hadithi kufundisha stadi za kusikiliza na kuzungumza, uliundwa mwongozo ambao unawasilisha mambo ya kuzingatia kwa kila hatua ya somo. Mapendekezo mbalimbali yametolewa kwa wadau mbalimbali ili kufanikisha uungaji mkono wa kutumia hadithi katika ufundishaji na ujifunzaji wa stadi za kusikiliza na kuzungumza kama stadi za msingi.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789