Main Article Content

Changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari za umma Tanzania: mfano wa shule teule za sekondari Wilaya ya Kwimba


Alcheraus R. Mushumbwa

Abstract

Ufaulu wa somo la Kiswahili kwa shule za sekondari za umma za Wilaya ya Kwimba ni hafifu ukilinganishwa na ufaulu wa somo hilo kitaifa. Hali hii ilibua mabunio ya kuwa huenda kuna changamoto katika ufundishaji na ujifunzaji zinazosababisha matokeo mabaya ya somo la Kiswahili kwa shule za wilaya hiyo. Hivyo, makala hii inachunguza changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari za umma zinazoweza kuwa sababu ya ufaulu hafifu wa somo hili. Utafiti ulioibua makala hii ulihusisha shule tatu za sekondari za umma. Kwa kuongozwa na Nadharia ya Utekelezaji Mtaala (Gross, 1971) na mkabala wa kitaamuli, makala inabainisha changamoto zinazokabili ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili zinazohusu lugha, miundombinu, taaluma/ujuzi, mtazamo hasi kwa Kiswahili, kimazingira na mamlaka. Aidha, mapendekezo ya kutatua changamoto hizo yametolewa kulingana na tafsiri ya data za makala ili kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika shule za sekondari za umma za Wilaya ya Kwimba.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789
 
empty cookie