Main Article Content

Vipengele vya kiontolojia vinavyounda jaala za mashujaa katika tendi za Nanga


Hellen Lyamuya

Abstract

Makala hii inachunguza vipengele vya kiontolojia vinavyounda jaala za mashujaa katika tendi za Nanga. Wataalamu waliotangulia hawajatilia mkazo nafasi ya ontolojia ya Kifrika katika kuunda jaala za mashujaa wa tendi za Kiafrika. Lengo la makala hii ni kuweka bayana vipengele vinavyounda jaala za mashujaa katika tendi za Rukiza na Mugasha. Makala hii imetumia utafiti wa maktabani na uwandani. Mbinu zilizotumika ni mbinu ya uchanganuzi wa matini na mahojiano. Sampuli ya utafiti ni wapiga Nanga, wazee na vijana wanaopatikana Mkoa wa Kagera. Matokeo ya uchunguzi uliofanywa yameonesha kuwa jaala za mashujaa wa tendi za Nanga zinaundwa na vipengele vya ontolojia ya Kiafrika kama vile kuthamini uzazi, kuheshimu wahenga, uanthropomofia, nguvu ya kani, umoja na mshikamano na uhusiano wa maumbile na vilivyomo.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789
 
empty cookie