Main Article Content

Nafasi ya kejeli katika tamthilia ya kaptula la marx: silaha muhimu ya kufikirisha, kukebehi na kufichua uozo


Saade Mbarouk

Abstract

Kejeli ni mbinu muhimu ya kifani inayochangia uandishi bora wa kazi za fasihi. Katika tungo bunilizi za fasihi andishi ya Kiswahili, kejeli ilianza kutumika katika karne ya 20, wakati waandishi wa mwanzo wa kazi bunilizi walipoonesha uwezo wao wa uandishi uliobeba vionjo makini vya kiujumi ili kuifikirisha hadhira na kuweka wazi matatizo ya jamii. Makala hii inalenga kuiangalia nafasi ya kejeli kama silaha muhimu ya kufikirisha hadhira, kukebehi na kufichua uozo unaotendeka ndani ya jamii. Uchambuzi wa makala hii umeongozwa na Nadharia ya Semiotiki iliyoendelezwa na mwanamuundo maarufu, Roland Barthes. Data zilikusanywa kupitia njia ya maktabani na uwandani kwa kutumia njia ya udurusu wa matini na mijadala ya makundi. Data zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya kitaamuli. Makala hii imebainisha na kufafanua nafasi ya kejeli zilizojitokeza katika tamthilia ya Kaptula la Marx katika miktadha ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii ambazo ni kukosoa, kukebehi, kudharau waovu, kufichua na kukemea uovu unaofanyika katika jamii, kama vile ufisadi, unyanyasaji, ubaguzi na kuburudisha hadhira.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789