Main Article Content

Uchanganuzi wa mbinu za kisarufi katika kampeni za uchaguzi: mifano kutoka uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015


Ahmad Yahya Sovu

Abstract

Madhumuni makuu ya ushawishi katika kampeni za uchaguzi ni kukubalika. Mara nyingi lugha inayotumika katika siasa ina lengo la kusifia au kulaumu. Lugha hiyo huwa yenye ubunifu, ya kujenga au kubomoa kwani hutumika kama silaha ya kujilinda. Kwa misingi hiyo, makala hii inachunguza matumizi ya mbinu za kiisimu katika kampeni za uchaguzi yanayowezesha kuvuta hisia na kuteka masikio ya hadhira. Aidha, Makala hii inabainisha na kujadili matumizi ya mbinu za kisarufi katika mikutano ya kampeni za uchaguzi wa Tanzania mwaka 2015. Uchunguzi umeongozwa na Nadharia ya Balagha na data zimekusanywa kupitia njia ya maktaba. Makala imebaini kuwa katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015, wanasiasa walitumia mbinu za uteuzi wa msamiati/istilahi maalumu, matumizi ya viwakilishi nafsi, ukanushi wa sentensi. Makala inatoa mchango mkubwa katika kuonesha nguvu ya lugha na ushawishi ya wazungumzaji wa kisiasa katika kufanikisha malengo yao ya kisiasa ambayo ni kushinda uchaguzi.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789
 
empty cookie