Main Article Content

Dhana potofu zilizopandikizwa na wageni kuhusu Afrika na Mwafrika: mifano kutoka riwaya teule za euphrase kezilahabi


Alfred Malugu
Ernest Sangai Mohochi
Mugyabuso Mlinzi Mulokozi

Abstract

Kwa muda mrefu kumekuwapo na dhana potofu kuhusu Afrika na Mwafrika. Kihistoria, suala hili linaweza kutazamwa kuanzia kipindi cha ukoloni. Msingi mkuu wa dhana hizi potofu kuhusu Afrika na Mwafrika ulijengewa msingi wake katika vitabu vya dini kama vile Biblia Takatifu, na pia mawazo ya wanafalsafa na wasomi maarufu wa kale wa Kimagharibi kama vile Carl Meinhof na Georg Hegel. Dhana potofu zilizopandikizwa zilichochea kutawaliwa kwa Waafrika na Afrika kwa jumla. Kutokana na kuwapo kwa dhana hizo, makala hii inakusudia kubainisha dhana potofu mbalimbali kuhusu Afrika na Mwafrika katika riwaya za Kezilahabi za Gamba la Nyoka, Nagona na Mzingile. Data kwa ajili ya makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi matini. Mbinu hii ilihusisha utoaji wa maelezo ya kina kuhusu dhana potofu mbalimbali kuhusu Afrika na Mwafrika. Aidha, katika kubainisha dhana hizo, tuliongozwa na baadhi ya mihimili ya Nadharia ya Ubaadaukoloni, ambapo miongoni mwa dhana potofu zilizopandikizwa zilijidhihirisha kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789