Main Article Content

Ndwele ielekezayo kwenye kifo katika Ua la Faraja na Kichwamaji


Matthew Kwambai
Issa Mwamzandi
Abdulrahim Hussein Taib Ali

Abstract

Ndwele ielekezayo kwenye kifo inatokana na hofu na usumbufu anaopata binadamu maishani. Ndwele hii ni sawa na utamaushi.  Binadamu anapitia mambo mengi katika maisha yake. Katika kusaka uhuru na kujitoa kwenye changamoto za maisha, anafanya uchaguzi mbalimbali. Uchaguzi na matokeo yake humfanya binadamu kuwa na hofu na usumbufu ambao, mwisho humsukuma awe na ndwele ielekezayo kwenye kifo. Ndwele hii inamfanya binadamu kufika kiwango ambacho anaepuka hatari anayofikiri ni kuu katika maisha yake. Akipatwa na hatari kuu anachagua kifo. Anapokabiliwa na kifo, anaona kuwa ni afadhali matatizo ambayo amekuwa akikumbana nayo. Lengo la makala hii ni kuangazia ndwele ielekezayo kwenye kifo katika Ua la Faraja (Mkufya, 2004) na Kichwamaji (Kezilahabi,1974) hasa kwa kutazama kiini chake na matokeo yake. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni ya Utamaushi ambayo iliasisiwa na Sartre (1966), inayoangazia kuwepo kwa binadamu duniani, matatizo anayopitia, utafutaji wa uhuru na mwisho kifo kama suluhu. Mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo ilitumiwa katika kuchambua data kwenye Ua la Faraja na Kichwamaji. Pia, mbinu hii ilitumiwa kuchambua makala mbalimbali kwenye maktaba na mtandao ili kuelewa suala la ndwele ielekezayo kwenye kifo. Matokeo katika utafiti huu yalionesha kuwa: kuna ndwele ielekezayo kwenye kifo katika Ua la Faraja na Kichwamaji. Kiini cha ndwele hii ni magonjwa, mahusiano, dhambi na kifo. Kuna Suluhu kwa hali hizi kupitia madhehebu ya Kikatoliki katika Kichwamaji na dini ya Kiislamu na mawaidha ya Dkt. Hans katika Ua la Faraja.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789
 
empty cookie