Main Article Content
Mantiki katika miiko ya mfumo-mlo ya jamii ya Wandendeule
Abstract
Makala hii inajadili miiko inayohusiana na mfumo-mlo katika jamii ya Wandendeule. Shabaha kuu ni kubainisha mantiki (kama kipengele kimojawapo cha falsafa) iliyomo ndani ya miiko. Swali kuu lililoongoza uchunguzi na mjadala wa kwenye makala hii ni: miiko kama kipengele cha kiutamaduni ina mantiki gani katika maisha ya wanajamii husika? Makala imejiegemeza katika mkabala wa kitaamuli. Data za makala hii zilipatikana kwa kutumia njia tatu ambazo ni udurusu wa nyaraka, usaili, pamoja na ushuhudiaji. Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa miiko yote inayohusu mfumo-mlo inayotumiwa na jamii ya Wandendeule hujikita katika mantiki fulani inayoshikilia seti ya 'kweli’ zinazoongoza maisha yao. Hii ni kwa sababu miiko hiyo huakisi uhalisi wa miktadha ya kimazingira (kijiografia), kijamii na kifikra (mawanda ya fikra zao kuhusu ulimwengu).