Main Article Content

Athari za valensia ya kitenzi katika usarufi wa miundo ya Kiswahili


Mosol Kandagor
Salim Sawe

Abstract

Wasemaji wa lugha huzingatia aina tatu za kanuni za uzuifu madhubuti zinazofungamana na valensia ya kitenzi katika uundaji wa sentensi za Kiswahili. Katika mkabala huo basi, makala hii inatambuai kwamba kanuni husika hubainika kwa sababu baadhi ya vijenzi (hasa nomino) vikiondolewa au vikiongezwa kwenye uambajengo wa kisintaksia, miundo isiyofasilika huzalishwa. Uchanganuzi unaofanywa katika makala hii unaonesha kwamba ufasili hauwezekani iwapo taarifa za kutosha hazitawakilishwa kwa wasikilizaji au ikiwa taarifa zisizofaa zitashirikishwa kwenye sentensi. Aidha, makala hii inaonesha kwamba kanuni tatu za uzuifu madhubuti ambazo ni za kanuni ya uzuifu wa valensia moja, kanuni ya uzuifu wa valensia mbili na kanuni ya uzuifu wa valensia tatu huhusu idadi ya nomino zinazohitajika kwenye muundo kwa mujibu wa kitenzi kilichotumiwa.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789