Main Article Content

Muziki wa Hip Hop na Haki Za Kijamii: Dhima, Changamoto na Mapendekezo


H Jilala

Abstract

Haki za kijamii ni suala ibuka na la msingi kumakinikiwa katika uchunguzi na uchambuzi wa kazi za fasihi. Ni jambo ambalo linahitaji kujadiliwa na kuelezewa kwa jicho la kisanii. Sanaa ina nguvu sana katika kuelimisha, kuonya, kuadili, kuhamasisha, na kufunza. Ni dhahiri kuwa haki za kijamii zinaweza kuwasilishwa kwa jamii pana kupitia sanaa ya hip hop. Makala haya basi, yanabainisha dhima na mchango wa muziki wa hip hop katika masuala ya haki za kijamii, yanafafanua changamoto za muziki huu katika kuwasilisha haki za kijamii na kutoa mapendekezo kwa makundi husika.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-6739