https://www.ajol.info/index.php/eajk/issue/feedEastern Africa Journal of Kiswahili2024-10-20T12:28:45+00:00Dr Michael Ndonye, PhDeditonltd@gmail.comOpen Journal Systems
Eastern Africa Journal of Kiswahili (ISSN 2958-1036) is a double-blind peer reviewed, open access, online Journal published by Editon Consortium Publishing, East Africa, Kenya. The Journal publishes original scholarly research (empirical and theoretical), in form of case studies, reviews and analyses in Kiswahili Linguistic Studies.

Aims and Scopes

The Journal publishes original scholarly research (empirical and theoretical), in form of case studies, reviews and analyses in Kiswahili Linguistic Studies.

You can see the journal's own website here.
https://www.ajol.info/index.php/eajk/article/view/281148Matumizi ya umajazi wa kitashtiti katika usawiri wa wahusika na maudhui katika riwaya: Mfano wa riwaya ya Tumaini2024-10-20T11:54:24+00:00Dave Bowentbowenza@yahoo.com
Makala hii iliazimia kuhakiki matumizi ya mbinu ya umajazi wa kitashtiti katika kukuza wahusika na kuendeleza maudhui katika riwaya ya Tumaini ya Clara Momanyi. Madhumuni ya karatasi hii ni kuchanganua namna mbinu ya umajazi wa kitashtiti umetumiwa kuwakuza wahusika na kuendeleza maudhui katika riwaya ya Tumaini. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Umuundo. Wataalamu kama Scholes na Olsen wanashikilia mawazo kwamba ni muhimu kutumia Umuundo katika uhakiki wa maandishi ya fasihi kwa sababu lugha na fasihi zina uhusiano mkubwa sana. Matumizi ya Umuundo katika uhakiki wa fasihi hutuelekeza kuitazama fasihi kama mfumo ambao unajumlisha vipengele kama: Fani na maudhui ambavyo huchangia ukamilifu wake. Vipengele hivi huchangiana na kukamilishana katika kazi ya fasihi kama vile riwaya. Nadharia hii ya Umuundo ilitusaidia kuhakiki namna mbinu ya umajazi wa kitashtiti umetumiwa kusawiri wahusika na kuendeleza maudhui katika riwaya ya Tumaini. Ukusanyaji wa data ulifanyika maktabani. Riwaya teule na makala zinazohusiana na mada zilisomwa. Data zilidondolewa, zilichujwa, zilichunguzwa na kisha zilichanganuliwa kwa kutumia majedwali na asilimia ya majina ya majazi ya kitashtiti. Data zilizokusanywa pia zilitumiwa kuhakiki matumizi ya umajazi wa kitashtiti katika kuwakuza wahusika na kuendeleza maudhui katika riwaya ya Tumaini. Pia, tuligundua kwamba mbinu ya matumizi ya umajazi wa kitashtiti yana mchango mkubwa kuwasawiri wahusika na kuyaendeleza maudhui katika riwaya ya Tumaini. Aidha, matokeo ya utafiti huu yatasaidia wahakiki, waandishi, walimu na wanafunzi wa shule za upili na hata vyuoni kuhakiki matumizi ya majina ya kimajazi katika kazi za fasihi andishi. Mbali na kazi hii kuwafaidi wahakiki, matokeo ya utafiti huu yatakuwa na mchango mkubwa katika kuwahamasisha waandishi chipukizi kutumia mbinu ya umajazi wa kitashtiti katika harakati zao za utungaji riwaya.
2024-10-20T00:00:00+00:00Copyright (c) 2024 https://www.ajol.info/index.php/eajk/article/view/281150Uchanganuzi wa mielekeo ya wanafunzi kuhusu ufundishaji wa Stadi za Mawasiliano kwa Kiswahili katika taasisi za kiufundi za kitaifa nchini Kenya kwa misingi ya michepuo ya masomo2024-10-20T12:00:46+00:00Jackson Mutuku Kavoi jkavoi@kabarak.ac.ke
Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchanganua mielekeo ya wanafunzi wa kozi za sayansi na sanaa kuhusu ufundishaji wa Stadi za Mawasiliano kwa Kiswahili nchini Kenya. Aidha, kuchunguza visababishi vya mielekeo husika kuhusu umuhimu wa matumizi ya Kiswahili kufundisha stadi za mawasiliano. Muundo wa Uchunguzi Kimaelezo ulitumiwa, huku taasisi 5 za kiufundi za kitaifa na sampuli ya wanafunzi 148 wakishirikishwa katika utafiti. Fomula ya Balian (1988) ya uteuzi wa sampuli ilizingatiwa na ukusanyaji wa data ulitumia kitanga cha mielekeo ya hojaji ya Likert kilichokarabatiwa, maswali ya wazi na dodoso. Waaidha, Zanatepe ya Kichanganuzi Data ya Kitakwimu za Sayansi Jamii (SPSS) kilitumika kuchanganua data. Matokeo yalidhihirisha kuwa, asilimia 2.82 ya wanafunzi 142 waliohusishwa katika uchanganuzi walidhihirisha mielekeo hasi, ilhali asilimia 97.18 walionyesha mielekeo chanya kuhusu ufundishaji wa Stadi za Mawasiliano kwa Kiswahili katika taasisi za kiufundi nchini Kenya. Aidha, wanafunzi wa kozi za sanaa walidhihirisha mielekeo chanya ya chini wakilinganishwa na wenzao wa sayansi. Uchanya huu ulitokana na faida ya utoaji wa huduma uwandani kwa wateja wao waliyoiambatanisha na kuridhia Kiswahili kitumike katika ufundishaji wa stadi za mawasiliano. Kwa mkabala huu, wanafunzi wa taasisi husika waliona umuhimu wa mawasiliano kabambe katika utoaji huduma nyanjani. Hivyo, kuanzishwa kwa ufundishaji wa stadi za mawasiliano kwa kutumia Kiswahili sambamba na Kiingereza kungewasaidia kuchonga maarifa yaliyogusia mawasiliano. Matokeo ya utafiti huu ni ya umuhimu kwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia na Taasisi ya Ukuzaji wa Mitaala, Kenya katika utungaji wa sera ya elimu katika taasisi husika.
2024-10-20T00:00:00+00:00Copyright (c) 2024 https://www.ajol.info/index.php/eajk/article/view/281151Teknolojia ibuka na ufundishaji wa somo la Kiswahili2024-10-20T12:08:50+00:00Anyonje M. Florenceanyonjeflorence@gmail.comMilton Kigaro Lihandaanyonjeflorence@gmail.com
Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchanganua teknolojia ibuka na ufundishaji wa somo la Kiswahili. Katika sekta mbalimbali kama vile afya, benki, biashara, usafiri, utawala, kilimo, ufundi na hata mawasiliano teknolojia za kisasa zinatumiwa. Sekta ya elimu haijaachwa nyuma katika matumizi ya teknolojia hizi. Utafiti huu ulizingatia nadharia ya Piaget inayosema kuwa akili ya mtoto hukua kulingana na mtagusano wake na mazingira. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa, Teknolojia ibuka kama vile mtandao, tarakilishi, video, redio, simu, setelaiti, barua pepe, runinga, vipakatalishi, zote zinaweza kutumiwa kurahisisha mawasiliano darasani, kujenga kumbukumbu ya wanafunzi, kuwapa nafasi ya kutafiti mada tofauti, kufurahia kujifunza, kupata uhalisa wa yale wanayojifunza na hata kufanyia mazoezi teknolojia tofauti kwa maandalizi ya ulimwengu wa kazi. Pia idadi ya wanafunzi inaendelea kupanda ikilinganishwa na waalimu wanaotakiwa kushughulikia wanfunzi hawa. Kwa vile Kiswahili ni somo la lazima teknolojia hizi zingekumbatiwa ingekuwa rahisi sana mwalimu kufunza stadi kwa wanafunzi wengi wakati mmoja hata wakiwa katika maeneo tofauti. Teknolojia ibuka huzingatia fahiwa tofauti hasa za kusikiliza na kuona. Redio, epurekoda, runinga, simu za mkononi zinaweza kutumiwa kufunza stadi ya kusikiliza. Tepurekoda, kanda za video, runinga zinaweza kutumiwa kufunza stadi ya kuzungumza. Stadi ya kusoma inaweza kufunzwa kwa kutumia mtandao, vifaa vya kurekodi sauti, nayo stadi ya kuandika inaweza kufunzwa kwa kutumia simu za mkononi, runinga, mtandao au video. Wanafunzi wanaweza kupata ujumbe, ufafanuzi kwa kutafiti mtandaoni. Inatarajiwa kuwa waalimu na wanafunzi wa somo la Kiswahili watazingatia teknolojia ibuka kuelewa somo hili na kupata umilisi wa kutumia lugha ya Kiswahili katika mawasiliano.
2024-10-20T00:00:00+00:00Copyright (c) 2024 https://www.ajol.info/index.php/eajk/article/view/281153Uchanganuzi wa vipashio vya mamlaka katika midahalo ya siasa za uchaguzi wa 2022 nchini Kenya kwenye jukwaa la kidijitali la youtube2024-10-20T12:14:27+00:00Aboge Nelson Asige naasige@gmail.comFrida Mirukanaasige@gmail.comAkinyi Juliet Jagero naasige@gmail.com
Makala hii inalenga kutambua mchango wa lugha kama chombo kinachodhihirisha mamlaka katika jamii kwa kuchanganua baadhi ya vipashio vilivyodhihirisha mamlaka katika midahalo ya wakati wa uchaguzi wa 2022 nchini Kenya kama inavyojitokeza katika jukwaa la kidijitali la Youtube. Wanasiasa wana hulka ya kutumia lugha yenye kupendeza kwa wananchi nyakati za kampeni kwa njia ya kipekee ili kubadilisha mawazo yao. Katika harakati hizi, wanasiasa huvuta mamlaka upande wao kwa njia isiyo wazi. Hali hii huwafanya wasikilizaji wengi kukosa kuelewa habari iliyotolewa kwa kutoelewa vipashio vilivyotumiwa katika hotuba hizo, hivyo kufanya maamuzi mabaya kisiasa. Utafiti huu ulizingatia muundo wa kiuchanganuzi kwa kutathmini data za kiuthamano zitakazoelezwa kinathari. Eneo la utafiti ni la kitaaluma. Kundi lengwa la utafiti ni midahalo ya wanasiasa wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka wa 2022 nchini Kenya. Usampulishaji wa kimaksudi ulitumika huku data zikikusanywa kutoka kwenye mtandao wa youtube kwa mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo na kuwasilishwa kimaelezo. Makala hii ilibainisha kuwa japo siasa huwasisimua wananchi na midahalo yake kuwavutia kwa wingi, wengi wao hukosa kuelewa kabisa wayasemayo wanasiasa hawa huku wengine wakipata ufasiri potovu. Data zilizokusanywa zitasaidia katika kudhihirisha sababu za wananchi kutoelewa habari fiche ambazo huwasilishwa na wanasiasa katika midahalo yao, ambacho ndicho chanzo cha wananchi kutoelewa habari hizo na hivyo kufanya maamuzi mabaya kwa kuwachagua viongozi wasiofaa.
2024-10-20T00:00:00+00:00Copyright (c) 2024